Header logo

Maelezo muhimu ya inDriver kuhusu homa ya korona (COVID-19)

Afya na usalama wa watumiaji wetu ni lengo letu kuu katika kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya korona (COVID-19). Kutokana na habari za karibuni juu ya janga la virusi vya korona, tunataka kuhakikisha kuwa watumiaji wa inDriver wanafahamishwa vizuri kuhusu njia bora ya kuzuia magonjwa, wakiwa katika safari za inDriver na katika maisha yao ya kila siku.

Kuhusu virusi vya korona (COVID-19)

COVID-19 ni jina la ugonjwa unaosababishwa na virusi vipya vya korona. CO = Korona, VI = Virusi, D = Ugonjwa, 19 = 2019 - mwaka ambao ugonjwa ulisajiliwa kwanza. Homa ya Korona ni familia ya virusi ambavyo husababisha dalili dhaifu, kama homa ya kawaida, na vile vile magonjwa mazito ya kupumua, kama vile nimonia. Tunawahimiza watumiaji wetu kutegemea habari za kuaminika tu kutoka kwa vituo rasmi vya Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Dumisha usafi wa kimsingi

Mara kwa mara safisha mikono yako na sabuni, na utumie sanitaiza inayotokana na alkoholi baada ya kugusa vitu.

Weka nafasi kati yako na wengine

Weka umbali wa angalau mita 3 kutoka kwa watu wengine, haswa ikiwa wana kikohozi au ugonjwa, joto la juu, au kunaonekana kuwa wagonjwa.

Epuka kugusa uso wako

Inapowezekana, usiguse macho, pua, au mdomo, kwani hii inafanya iwe rahisi kwa bakteria kusafiri kutoka kwa mikono yako kuingia ndani ya mwili wako.

Zingatia usafi unaofaa wa mfumo wa kupumua

Wakati unapokohoa au kupiga chafya, funika kinywa chako na pua kwa tishu, kitambaa, au kiwiko. Tupa tishu mara moja kwenye boti la takataka na kifuniko na ujipake sanitaiza ya mikono au uoshe mikono yako kwa sabuni.

Epuka ya kukaribiana sana na watu katika jamii

Tafadhali jaribu kujiepusha na maeneo ya umma. Usiondoke nyumbani isipokuwa kama ni lazima: jinsi unavyoepuka migusano na watu ndivyo unavoongeza uwezekano wa kutoambukizwa.

Tafuta matibabu

Ikiwa una joto la juu la mwili, baridi, au unakabiliwa na udhaifu au ugumu wa kupumua, tafuta msaada wa kitiba mara moja. Usiondoke nyumbani; badala ya hilo, omba simu ya nyumbani kutoka kwa daktari.