Header logo

Ruhusu hewa safi kwenye gari na uweke viua viini ndani ya gari lako

Fungulia hewa ndani ya gari lako angalau mara mbili kwa siku, na haswa baada ya kila abiria kutoka. Kufungulia hewa ndani ya gari lako si vigumu na hakutakuchokesha: Jambo la muhimu ni kutosahau kufanya hivyo. Na hewa safi, nzuri ni jambo bora katika hali yoyote!

Fanya usafi kutumia viowevu ndani ya gari kwa kutumia kiua viini mara kadhaa kwa siku. Tunapendekeza utumie kloramini B, peroksidi ya hidrojeni kwenye sehemu ya ndani, na bidhaa zinazotokana na alkoholi ya mkusanyiko wa angalau 70%, na pia amine na kiwango fulani cha polyhexamethylene guanidine. Zingatia kwa uangalifu milango, mikanda ya viti, vito vya visugudi, nyuma ya viti, na sehemu za ngozi na chuma ndani ya gari. Ukifuata pendekezo hili, utapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa ugonjwa wa virusi vya korona na maambukizi mengine.